Sababu za Maumivu Makali ya Mgongo


Kuna sababu  mbalimbali zinazoweza kupelekea maumivu ya
mgongo nazo ni;

1.  Maambukizi
katika pingili za uti wa mgongo
:
Maambukizi katika pingili za uti wa mgongo kama vile maambukizi ya saratani ya
mifupa huweza kuleta maumivu makali ya mgongo.

2.  Kuvunjika
kwa pingili za uti wa mgongo
:
 Hali hiii inaweza kusababishwa na vitu mbalimbali hususani ajali ya kuanguka au
kupinduka na gari.

3.  Umri
mkubwa:
Tatizo la maumivu ya mgongo mara kwa
mara huwakuta watu wazima na wazee.


4.  Uzito
kupita kiasi (Obesity)
:
Uzito wa mwili
kupita kiasi husababisha kuelemewa kwa uti wa mgongo na hivyo kuleta mgandamizo
wa pingili za uti wa mgongo na kusababisha maumivu makali ya mgongo.

5.  Kukaa
kwa muda mrefu:

Kukaa kwa muda mrefu kama vile ofisini au madereva bila ya mazoezi hupelekea
maumivu ya Mgongo.


6.   Mtindo Mbovu wa Maisha (Bad Lifestyles):
Mtindo wa maisha kama vile kupuuza mbogamboga na vyakula vya asili hupelekea
kuwa na mifupa hafifu na hivyo ni rahisi kuathirika hata kwa msuguo mdogo tu.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top