MAFUFA YA MAKONYO YA KARAFUU
Hutumika kutibu meno na fizi
Unusaji wa mafuta ya makonyo huondosha kizunguzungu na maumivu ya kichwa.
Husaidia kuongeza uwezo wa kumbukumbu na kuongeza mzunguko wa damu.
Pia yanaongeza uchangamfu,kuondosha vimbizi la tumbo na kuongeza za kiume,huhifadhi ngozi na kupunguza
kuchanganyikiwa na hata shinikizo la damu.
Hutumika kuondosha maumivu ya misuli,nyonga na maumivu ya mwili kiujumla.
NAMNA YA KUTUMIA MAFUTA YA ARKI YA MIMEA
NJIA YA KUVUTA PUMZI NA KUPUMUA.
Weka matone 3 hadi 4 ya mafuta katika karatasi ya
tissue au kitambaa cha mkononi na ukiweke chini ya pua yako.Vuta pumzi kwa nguvu kidogo na uone raha nzuri ya mafuta.
NJIA YA KUPUMUA NA KUVUTA PUMZI KWA KUTUMIA MVUKE.
Tia matone 3 katika bakuli la maji ya moto.Funika kichwa chako katika kwa kutumia taulo.Vuta mvuke wenye kutibu.
KUOGA MAJI YENYE MAFUTA KWENYE BAFU.
kwaajili ya kuchangamsha mwili,kupunguza msongo wa mawazo na maumivu ya misuli.kwa
kutumia mafuta haya husaidia kuondosha matatizo ya ngozi ,uchovu wa akili,matatizo ya neva
na misuli ya hedhi.
Chanaganya matone 6 ya mafuta na nusu kikombe cha chumvi ya kupikia.Changanya mafuta na chumvi katika bafu la maji yaliyojaa.Kwa ngozi iliyodhaifu punguza mafuta.
KUKANDA KWA KUTUMIA TAULO LA MOTO.
Tia matone kumi ya mafuta katika milimita 250 ya maji moto.Roweka taulo au kitambaa ndani ya maji hayo maji halafu kanda sehemu yenye meumivu kwa kutumia taulo lililoroana.
Matibabu haya ni mazuri kwa kutibu michubuko ya n gozimaumivu ya viungo ,vidonda ,,maumivu ya misuli.
KUSAFISHA USO KWA KUTUMIA MVUKE WA MAJI WENYE MAFUTA.
Tia matone 2-3 ya mafuta katika bakuli la maji ya moto.funika kichwa kwa kutuma taulo Waha uso usafishike kwa kupigwa na mvuke.
Matibabu haya ni mazuri kw akusafisha tundu za ngozi za uso na kutibu maradhi ya chunusi,kichwa na ngozi ya kichwa.
MATIBABU YA NGOZI NZNYWELE
Tone moja la mafuta lichanganywe na krimu isiyo na harufu au mafuta ya nywele au mafuta ya nazi n.k .Mafuta haya yachanganywe na vipodozi vya kupaka usoni.Tahadhari ichukuliwe kwa ngozi dhaifu.
MATIBABU YA MENO NA UFIZI
Chukua pamba kidogo na itie kiasi kidogo cha mafuta , itie pamba katika pango la jino au iumie kwa kukanda ufizi..





